LONDON, England
NYOTA wa Manchester United, Cristiano Ronaldo anaamini kwamba Bayern Munich ndio kikosi cha kukiogopa katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezajii huyo anakihofia kikosi kinachonolewa na Jurgen Klinsmann kwa kuwa kiliifunga Sporting Lisbon mabao 12-1 katika mechi za awali.
Ronaldo amebainisha kwamba amekuwa akikichunguza kikosi hicho cha Ujerumani, ambacho kilifungwa na Manchester United mwaka 1999 na kufanikiwa kuingia hatua ya fainali.
Alisema: "Niliwachunguza Bayern walipocheza na Sporting, wanaonekana ni wenye nguvu nyingi.