LOS ANGELES, Marekani
IMEFAHAMIKA kwamba baba wa Beyonce aitwaye Mathew Knowles ametimuliwa kazi ya umeneja wa mwanamuziki Lyfe Jennings.
Na badala yake Jennings amemsaka meneja mwingine aitwaye Manny Hailey, ambaye pia ni meneja wa Keyshia Cole.
Habari za uhakika zinasema kwamba Lyfe na Mathew walikorofishana katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kipato.
Mtu mmoja wa ndani alisema: "Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, Lyfe amefanikiwa kupata meneja ambaye wanapatana."
Hivi karibuni Mathew pia alitimuliwa kazi na Kelly na imefahamika kwamba Michelle pia anataka kuachana na baba huyo wa Beyonce.