Sep 9, 2010, 9:28 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2009-03-16 17:00:00
Kipa amuacha mkewe wa pili
LONDON, England
KIPA wa zamani wa Arsenal, David Seaman amemuacha mke wake wa pili ikiwa ni miaka 15 tangu alipoachana na mkewe wa kwanza.

Kipa huyo wa zamani wa England, ambaye alipewa jina la 'Mikono Salama' amewashangaza marafiki na ndugu zake kwa uamuzi huo.

Wikiendi hii, mke wa pili aliyeachwa aitwaye Debbie, ambaye ni mama wa watoto wawili (msichana na mvulana) alisema: "Kila mtu amechanganyikiwa lakini nina watoto wawili wazuri wa kuwalinda."

Mwaka 1994 gazeti la 'News of the World' liligundua kwamba Seaman ambaye sasa ana miaka 45, alimtelekeza mke aitwaye Sandra na watoto baada ya kuishi naye kwa miaka 10.

Ilielezwa kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal alikimbia nyumba yake na kumuacha mkewe na watoto wawili Daniel na Tommy, wakati huo wakiwa na umri wa miaka saba na nane.

Waandishi wa gazeti hilo walimnasa mchezaji huyo akiondoka nyumbani kwake London kwa siri akiwa na mabegi mawili. Msemaji wa Seaman alisema kuwa kwa mara nyingine ameikimbia familia yake.

Alisema: "David ameikimbia familia yake kwa mara nyingine wiki chache zilizopita, tumejaribu kuweka mambo sawa lakini tumeshindwa, mawakili wanaoshughulikia talaka bado hawajaitwa lakini ndio kitu kinachofuata."

Rafiki yake wa karibu alisema: " Suala hilo ni kama kipindi cha nyuma wakati alipomtelekeza Sandra, hatukufahamu kama anaweza kurudia kitendo hicho lakini amerudia."
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=1366