Sep 9, 2010, 9:23 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2009-03-16 16:58:00
Arshavin mwendo mdundo
LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba mchezaji Andrey Arshavin wa Russia ni hazina kwa klabu.
Arshavin amekuwa akijiweka fiti tangu alipojiunga na kikosi hicho katika dirisha dogo la usajili wa mwezi Januari.

Imeonekana kwamba mshambuliaji huyo ameanza kukaa sawa baada ya kupachika mabao mawili wakati timu yake ilipotoka kifua mbele kwa mabao 4-0 dhidi ya Blackburn Rovers.

Wenger alisema: "Alicheza kwa juhudi, nadhani hata yeye ameshangazwa na uwezo aliouonyesha.

"Lakini ninadhani kwamba ni mtu anayependa changamoto kwa kuwa alidiriki kuondoka St Petersburg, ambako alikuwa nyota na kufika England akiwa na umri wa miaka 28 inaonyesha ana uhakika na anachokifanya.

"Ninapenda wachezaji kama hao kwa sababu katika hatua ya mwisho wanaweza kukusaidia. Nadhani kila mchezaji anatakiwa kuwa na ari kama hiyo mpaka mwisho wa msimu.

"Lakini hata sisi tumewahi kuwauza wachezaji wetu kama Alexander Hleb na Tomas Rosicky,ambao walikuwa na miaka kati ya 27 na 30, waliamini kwamba wanaweza kufanya vema mbele ya safari.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=1364