Sep 9, 2010, 9:27 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2009-03-17 05:33:00
Rafa: Fergie chamtoto
Rafael Benitez wa Liverpool
LONDON, England
KOCHA wa Liverpool, Rafa Benitez amemwambia Alex Ferguson kwamba ataendelea kuwa 'baba yake' katika soka.

Benitez alimwambia kocha huyo wa Manchester United kuwa sasa Liverpool ni timu kubwa: "Liverpool ni timu kubwa ya Ulaya!"

Kocha huyo wa Liverpool amefurahi baada ya kuona akitoa kichapo kwa mabingwa wa Ulaya kwa jumla ya mabao 4-1 katika Uwanja wa Old Trafford.

Benitez aliongeza: "Liverpool imekuwa ni timu bora ya Ulaya kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo. Hilo lipo wazi.
"Sasa tunajiamini, tuna nguvu kubwa. Tunatakiwa kushinda kila mechi kuanzia sasa ili tuone nini kitatokea kwao."

Benitez amepania kumkosesha raha Ferguson na amesema kwamba kitendo cha kuwafunga kwenye uwanja wao wa nyumbani kimemchanganya.

Na kocha huyo wa Liverpool, ambaye aliwahi kukifunga kikosi hicho katika mechi ya awali msimu huu anaona kwamba ana kila sababu ya kumtawala Ferguson.

Benitez alisema: "Ninamheshimu Alex Ferguson, ni kocha bora lakini ninatakiwa kuitetea klabu yangu.

"Wakati mwingine Kiingereza changu si kizuri lakini sielewi vizuri lafudhi ya Scotland."

Ijumaa iliyopita Ferguson alisema kwamba alitakiwa kusoma filosofia za Sigmund Freud ili kumuelewa Benitez.

Benitez aliongeza: "Ni kweli nilijifunza kuhusu Freud wakati nilipokuwa shule ya awali na chuo kikuu.

"Nilijaribu kuongea Kingereza changu na ninadhani Ferguson atanielewa ninachozungumza baada ya mechi ya Jumamosi."

Kocha huyo anaamini kwamba Liverpool ina uwezo wa kushinda mechi zote zilizobaki na hatimaye kuibuka na ushindi.

Kocha huyo kutoka Hispania alisema: "Tunacheza vema, inabidi tufurahie maisha hayo na kuendelea kupata pointi tatu katika kila mechi."

Lakini kocha huyo anafahamu kwamba, iwapo Liverpool inataka kuhakikisha inaibuka na ushindi kila mara inabidi itumie kiasi kikubwa cha fedha katika usajili.

Benitez alisema: "Lengo la klabu yetu ni kupata ushindi na kuibuka na ubingwa, lakini Mancheter United pia wanataka jambo hilo.

"Katika maisha ya sasa ya soka, fedha inaweza kukufanya uwe na kikosi imara zaidi.

"Unaweza kuona jambo hilo wakati wa kubadilisha wachezaji uwanjani, kama katika benchi huna watu wazuri ni vigumu kufanikiwa."

Sigmund freud ni miongoni mwa wataalamu anayesifika kwa kuandika vitabu mbalimbali vya matatizo ya akili ya binadamu na jinsi maisha ya utotoni yanavyoathiri maisha ya mtu ukubwani.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=1363