Kaka amwaga chozi uwanjani

Muktasari:

Mchezaji huyo mwenye miaka 35 alitangaza kutorejea kikosini hapo mwakani.

Marekani. Mshindi wa zamani wa Ballon d’Or, Kaka ameaga kutoichezea timu yake ya Orlando City, huku akikosa bao kutokana na faulo aliyopiga wakati wa mechi dhidi ya Columbus Crew aliyoitumia kuaga Jumatano iliyopita.
Mchezaji huyo mwenye miaka 35 alitangaza kutorejea kikosini hapo mwakani.
Kaka alikuwa na Orlando City tangu mwanzoni mwa mwaka 2015 na alifanikiwa kufunga bao zuri bao lililoweka rekodi.
Hata hivyo, mchezaji huyo raia wa Brazil hatarajiwi kucheza mechi inayofuata ambayo timu yake itakutana na Philadelphia Jumapili ijayo.
Ligi hiyo ya Marekani inaelekea ukingoni huku Orlando ikiwa imekusanya pointi 39 huku vinara wa Ligi hiyo Toronto FC wakiwa na pointi 68.