Mario Balotelli apata mtoto

Muktasari:

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City, kwa sasa atakuwa na watoto wawili ambapo wa kwanza alizaa na mpenzi wake wa zamani, Raffaella Fico.

Mshambuliaji wa Nice, Mario Balotelli (27) ametuma picha akiwa na kichanga ambapo ni muda mfupi kabla ya klabu yake kushuka uwanjani kwenye mechi ya Ligi ya Europa.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City, kwa sasa atakuwa na watoto wawili ambapo wa kwanza alizaa na mpenzi wake wa zamani, Raffaella Fico.
Inasemekana mchezaji huyo mwenye miaka 27 amepata mtoto huyo wiki tatu zilizopita na amezaa na mpenzi wake wa sasa anayeitwa Clelia. Hata hivyo licha ya kutuma picha hizo, Balotelli hajazungumzia chochote kuhusu ujio wa malaika huyo.