Real Madrid yafunia orodha ya wachezaji 500 wenye mvuto duniani

Muktasari:

Katika orodha hiyo ya wachezaji 500 wenye mvuto, Real Madrid imetoa wachezaji19, hakuna klabu nyingine iliyowakaribia.

Madrid, Hispania. Real Madrid imetawala katika orodha ya wachezaji 500 wenye ushawisho mkubwa duniani iliyotolewa na jarida la World Soccer.

Katika orodha hiyo ya wachezaji 500 wenye mvuto, Real Madrid imetoa wachezaji19, hakuna klabu nyingine iliyowakaribia.

Wachezaji wa Real walioingia katika orodha hiyo ni Keylor Navas, Dani Carvajal, Sergio Ramos, Raphael Varane, Pepe, Nacho, Marcelo, Casemiro, Toni Kroos, Luka Modric, Isco, Marco Asensio, Mateo Kovacic, James Rodriguez, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Karim Benzema, Alvaro Morata na Jesus Vallejo.'

Bayern Munich ipo nafasi ya pili ikiwa na wachezaji 14, wakati Barcelona ikiwa nafasi ya tatu pamoja na Chelsea na Juventus zenye wachezaji13 kila moja.

Marc-Andre ter Stegen, Jordi Alba, Samuel Umtiti, Gerard Pique, Sergi Roberto, Ivan Rakitic, Andres Iniesta, Sergio Busquets, Andre Gomes, Paco Alcacer, Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez  ndiyo wachezaji waliochaguliwa kutoka Barcelona.

Atletico Madrid ipo nafasi ya sita ikiwa na wachezaji 12 sawa na Borussia Dortmund.

Walioingia kutoka Atletico ni Jan Oblak, Juanfran, Filipe Luis, Diego Godin, Jose Gimenez, Yannick Carrasco, Fernando Torres, Gabi, Kevin Gameiro, Koke, Saul na Antoine Griezmann.

Kwa ujumla LaLiga ina wachezaji 66 katika orodha ya wachezaji 500 mashuhuri, wakifuatiwa na Bundesliga (64), Premier League (63) na Serie A (60).