Bale bado yupo yupo sana tu Real Madrid

Madrid, Hispania. Pamoja na kuwepo kwa taarifa kuwa siku za Gareth Bale ndani ya Real Madrid zinahesabiki, hata hivyo kocha Zinedine Zidane anaona nyota huyo hagusiki hivyo hawezi kuondoka kwa sasa.

Mchezaji mwenyewe anataka kuendelea kuwepo Estadio Santiago Bernabeu, baada ya kuonyesha mchango wake katika timu hiyo katika msimu uliopita.

Alianza msimu vizuri, lakini majeruhi yalimuondoa mchezoni na hali hiyo hata hivyo inaaminika baada ya kupona atarejea katika ubora wake msimu ujao.

Pia, utata kuhusu hatma ya Cristiano Ronaldo ndani ya Madrid jambo lingine linaloonyesha umuhimu wa nyota huyo wa zamani wa  Tottenham Hotspur katika kikosi cha sasa cha Real 'Los Blancos'.

Mkataba wa Bale ndani ya Bernabeu utamalizika 2022, nyota huyo anaweza kuongeza mkataba huo akiwa hana nia ya kutaka kuondoka katika klabu hiyo.