#WC2018:Staa wa Tunisia kutulia kideoni tu

Muktasari:

Msakni (27), aliumia kwenye mecho wa ligi ya Qatar (QSL), ambapo timu yake ya Al Duhail iliitandika Al Sailiya mabao 5-2 mwishoni mwa wiki iliyopita.

KAMA kuna vitu ambavyo wachezaji mastaa wanakimbia basi ni kucheza na wachezaji ambao hawana nafasi ya kwenda Russia. Kila mchezaji anakwepa kuumia ili kutimiza ndoto yake ya kukipiga kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018. Lakini, nyota wa timu ya Taifa ya Tunisia, Youssef Msakni atazisikia fainali hizo baada ya kupata majeraha ya goti yatakayomuweka benchi miezi sita.
Msakni (27), aliumia kwenye mecho wa ligi ya Qatar (QSL), ambapo timu yake ya Al Duhail iliitandika Al Sailiya mabao 5-2 mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo, nyota huyo atakuwa na kitu cha kujivunia baada ya klabu yake kubeba ubingwa wa QSL, ambapo alitupia picha na maelezo kwenye ukurasa wake wa Instagram kuelezea hisia zake na kuthibitisha majeraha yake.
Akiwa na kikosi cha Tunisia, Msakni ametikisa nyavu mara tisa, ukijumlisha mabao matatu (hat-trick) aliyofunga dhidi ya Guinea na kuiwezesha nchi yake kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018