#WC2018:Neymar na wenzake watapeta tu hapa

Muktasari:

Lakini, kuna kundi jingine la wachezaji ambao ni mahasimu kwenye timu zao za klabu, lakini watakwenda Russia kuwa marafiki kwa sababu watakuwa kwenye timu moja kama ilivyo kwa Luka Modric na Ivan Rakitic, ambao mmoja ni Real Madrid na mwingine ni Barcelona kama walivyopangwa kweny mtiririko. Huo ndio utamu unaosubiriwa kwenye fainali hizo za Russia. Unajua jinsi timu zilivyopangwa kwenye makundi yao kwenye fainali hizo? Nakwambia moto utawala.

MOSCOW, RUSSIA
JOTO la Kombe la Dunia 2018 linazidi kupanda huku kila mchezaji ambaye timu yake imefuzu kwa fainali hizo za Russia akijaribu kujiweka sawa ili achaguliwe kwenye kikosi akaonyeshe makali yake. Ni fainali ambazo zinakwenda kuwafanya marafiki kuwa maadui au maadui kuwa marafiki kwa maana ya kwamba kuna wachezaji wanaocheza timu moja za klabu, lakini timu zao za taifa ni tofauti na watakwenda kukutana kwenye fainali hizo. Lakini, kuna kundi jingine la wachezaji ambao ni mahasimu kwenye timu zao za klabu, lakini watakwenda Russia kuwa marafiki kwa sababu watakuwa kwenye timu moja kama ilivyo kwa Luka Modric na Ivan Rakitic, ambao mmoja ni Real Madrid na mwingine ni Barcelona kama walivyopangwa kweny mtiririko. Huo ndio utamu unaosubiriwa kwenye fainali hizo za Russia. Unajua jinsi timu zilivyopangwa kwenye makundi yao kwenye fainali hizo? Nakwambia moto utawala.

KUNDI E

Timu zinazounda kundi:
Brazil
Uswisi
Costa Rica
China

Utamu kamili
Inavyoonekana Brazil hawatakuwa na kikwazo chochote kwenye kundi hilo na kwamba watatinga tu hatua ya mkoano bila ya ugumu wowote. Hilo linatokana na namna timu hiyo ilivyofuzu kwa kishindo fainali hizo na pamoja na ubora wa mastaa waliopo kwenye kikosi chao na kiwango cha wapinzani wao waliopangwa pamoja.
Kocha wa Brazil, Adenor Bacchi maarufu kama Tite ameibadilisha timu hiyo yangu alipoanza kuinoa Septemba 2016 na kukifanya kikosi hicho kucheza soka la kiwango kikubwa na kurudisha kipindi kile cha Samba lenyewe. Brazil itakwenda kwenye fainali hizo ikiwa na kikosi matata kwelikweli chenye mastaa kama Neymar, Philippe Coutinho, Gabriel Jesus, Casemiro, Paulinho, Willian na wakali wengine kibao. Brazil pia itakwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa 7-1 na Ujerumani katika fainali zilizopita zilizokuwa zimefanyika kwenye ardhi ya nchi yao huko Amerika Kusini. Kwenye kundi lao, mabeki wa Brazil watakuwa na kasheshe la kuwadhibiti mastaa kadhaa wa maana akiwamo Xherdan Shaqiri na viungo watakuwa na kazi ya kupambana na fundi wa mpira Granit Xhaka.

Ratiba ya Kundi E
Jumapili, Juni 17 - Costa Rica vs Serbia, Samara
Jumapili, Juni 17 - Brazil vs Uswisi, Rostov-on-Don
Ijumaa, Juni 22 - Brazil vs Costa Rica, Saint Petersburg
Ijumaa, Juni 22 - Serbia vs Uswisi, Kaliningrad
Jumatano, Juni 27 - Serbia vs Brazil, Moscow
Jumatano, Juni 27 - Uswisi vs Costa Rica, Nizhny Novgorod