#WC2018: Kocha Cherchesov kuiongoza kibabe Russia

Tuesday June 12 2018

 

Kikosi cha Russia kitaongozwa na kocha Stanislav Cherchesov aliyechukua mikoba kutoka kwa Lenonid Slutsky aliyejiuzulu nafasi ya kocha mkuu baada ya kufanya vibaya kwenye Euro 2016 hatua ya makundi.
Mara ya mwisho Russia ilishinda mechi kubwa mwaka Oktoba 2015 ambayo ni mashindano ya Kombe ya Shirikisho.
 Kwa mantiki hiyo unaweza kuipa nafasi finyu kwenye Kombe la Dunia msimu huu, kutokana na kuwa ni timu ambayo haipewi nafasi kubwa kufanya vyema kwenye mashindano hayo.
Timu hiyo ilizitangulia kufuzu timu za Uruguary na Misri kwenye kundi lake ikiwa ni historia nzuri kwenye mashindano hayo ya Kombe la Dunia  na iwapo itavuka hatua ya mtoano itakuwa ni mafanikio makubwa kwa timu hiyo mwenyeji.
Iwapo wachezaji hawatakuwa na ubunifu na mbinu zaidi kunaweza kuwafanya wakaaga mapema kwenye kundi A.