#WC2018:Joe Hart ndio basi tena England

Muktasari:

Hart ndiye aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Taifa ya England, lakini kwa sasa amepoteza nafasi hiyo kutokana na kushindwa kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha West Ham.

LONDON ENGLAND
HUKO England hakusomeki kabisa na kipa wa West Ham United, Joe Hart amekubali yaishe baada ya kufichua kuwa hafahamu lolote kuhusu fainali zijazo za Kombe la Dunia na badala yake anafikiria klabu yake tu.
Hart ndiye aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Taifa ya England, lakini kwa sasa amepoteza nafasi hiyo kutokana na kushindwa kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha West Ham.
Kauli ya Hart inachukuliwa kama kipa huyo amekata tamaa mbele ya Jordan Pickford  wa Everton, ambaye ameonekana kuwa chaguo la kwanza kwa kocha, Gareth Southgate.
“Kwa sasa mawazo yangu yote yapo kwenye klabu (West Ham) ambayo tunapigania nafasi ya kubaki Ligi Kuu, hivyo hakuna kitu kingine ninachofikiria kwa sababu hii ndiyo kazi yangu kwa sasa,” alisema Hart.