VIDEO: Kashkash za siku 30 zimemalizika Russia

Muktasari:

  • Croatia ilihitaji penalti mbili tu kufuzu fainali hizo baada ya muda wa ziada dhidi ya England na kukata tiketi ya fainali.

Moscow, Russia. Kabla ya fainali, mechi 63 zimepigwa na leo Julai 15, siku ya 30 Fainali za Kombe la Dunia 2018 zinafungwa na Ufaransa na Croatia zilikuwa zinakamilisha bonanza hilo la Moscow.
Kila mmoja amepita na njia yake kufikia Uwanja wa Luzhniki ikiwa ni fainali yake ya tatu katika miaka 20.
Croatia ilihitaji penalti mbili tu kufuzu fainali hizo baada ya muda wa ziada dhidi ya England na kukata tiketi ya fainali.
Mechi kama hizi za fainali mara nyingi ni makosa huamua mchezo, Lakini nani atafanya kosa na kupoteza mchezo? Ni wazi kila mmoja atakuwa makini katika hili.

Benjamin Pavard vs Ivan Perisic
Pavard alikuwa mtamu zaidi ya Hazard katika nusu fainali. Lakini Perisic ni kati ya wachezaji wakali wanaoweza kulitia njaa lango la Ufaransa, katika mechi ya England alifunga bao moja na akatoa asisti moja.
Mshambuliaji huyo wa Inter Milan alifanya vizuri katika mechi za utangulizi lakini katika mechi na England, alifunga bao murua.
N’Golo Kante vs Luka Modric na Kante watakuwa na shughuli moja katika dimba la kati juu katika kupandisha mashambulizi. Kante amekuwa kimya kwelikweli lakini amepiga mpira mkubwa hakuna.  
Kante ameisaidia sana Ufaransa katika kutibua mashambulizi ya wapinzani na ndiyo maana ngome ya Ufaransa haikuwa na kazi sana, na ndiyo sababu kubwa kwa timu hiyo kufanya vizuri katika mechi zake sita. Pamoja na Paul Pogba wamepandisha mashambulizi mengi langoni kwa wapinzani wao. Katika mechi za karibuni, Pogba amecheza soka la maana kiasi cha Juventus na Barcelona kuanza kumpigia hesabu kali.
Modric kwa upande wake ni kati ya wachezaji wanaowania Golden Ball. Ameibeba kwa kiasi kikubwa Croatia ikiwemo kuifikisha fainali.
Straika huyo wa Real Madrid amekuwa msaada mkubwa wa kikosi cha Zlatko Dalic na hata katika mechi na England. Muda ukifika mambo yatakuwa hadharani, nani ni nani.