VIDEO: Mashabiki wa Ufaransa wajipanga kurudi na Kombe la Dunia

Timu ya Ufaransa imekata tiketi ya kutinga ya kutinga 16 bora baada ya kuifunga Peru bao 1-0 kwenye mchezo uliofanyika jana Alhamisi, huku Peru wakijiandaa kurudi nyumbani baadaa ya kupoteza mchezo huo muhimu kwao.

Baadhi ya mashabiki wa Peru waliondoka uwanjani hapo na kubadilishana jezi na wenzao wa Ufaransa huku wengine wakionekana kuendelea kuangua kilio baada ya kuondolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia Russia.

 Kylian Mbappe alifunga bao lake la kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia tangu aanze kusakata na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuifungia timu ya taifa ya Ufaransa katika michuano hii ya Kombe la Dunia.

Straika huyo wa  Paris Saint-Germain, amevunja rekodi ya muda mrefu iliyowekwa na nyota wa zamani wa France, David Trezeguet, iliyodumu kwa miaka 20. Trezeguet alifunga bao lake katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 1998, yaliyofanyika nchini Ufaransa akiwa na miaka 20.

Mashabiki wa Ufaransa hawakusita kuonyesha furaha yao baada ya mchezo kumalizika huku wakisifu kikosi hicho kutokanna soka waliloonyesha. Hata hivyo waliweka bayana kuwa kikosi hicho kuna mamabo kadhaa ya kiufundi ambayo wanatakiwa kuyafanyia kazi hasa safu ya ulinzi.

Peru tayari wameshatolewa kwenye mashindano hayo na watacheza mchezo wao wa mwisho na Australia, huku Ufaransa watacheza mchezo wao mwingine dhidi ya Denmark  Juni 26.