VIDEO: Mashabiki Croatia wachekelea kumpoteza Messi

Mashabiki wa Croatia wametoa onyo kwa timu yoyote itakayokatiza kwenye anga zao kuwa wataumbuka kama walivyowanyoosha Argentina baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mchezo huo uliopigwa jana Alhamisi saa tatu usiku ilishuhudiwa kikosi cha Argentina kikiondoka patupu baada ya kuchezeshwa kwata.

Matumaini ya Argentina yalianza kufifia baada ya kutandikwa bao la pili, huku Lionel Messi akifika mara kadhaa kwenye lango la Crotia na pasi zake hazikuwa na madhara yoyote.

Uzembe wa kipa wa Argentina ulizamisha jahazi lao kwa kusababisha bao la pili la kizembe wakati alipokuwa akianzisha mpira kwa mabeki wake.

Mashabiki wa Croatia walidai bila shaka Argentina ilionyesha kiwango dhaifu ndiyo sababu ya kuruhusu mabao matatu kutinga wavuni kwao.

Hata hivyo mashabiki wa Argentina licha ya kuwa na pointi moja bado wanamatumaini ya kufanya vyema mchezo wao unaofuata.