Mashabiki wa Iran wajipa moyo kuitoa jasho Hispania

Mashabiki wa Iran wamesema kwamba wanafuraha kutokana na mchezo ambao kikosi chao kimeonyesha licha ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Hispania mechi iliyochezwa jana Jumatano usiku.

Mashabiki waliokuwapo uwanjani walionekana kuwapa sapoti kubwa timu ya Iran jambo ambalo lilisababisha uwanjana kuwa na kelele wakati wote huku mavuvuzela yakitawala dakika zote 90.

Baadhi ya mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo baada ya mchezo walielezea furaha yao kutokana na mchezo wa ushindani walionyesha licha ya kupokea kipigo, bao pekee ambalo lilifungwa na Diego Costa katika dakika ya 54 kiopindi cha pili.

Iran ilicheza kufa na kupona kuhakikisha inaibuka na ushindi, matumaini yao yalizikwa baada ya teknolojia ya video kuonyesha kuwa bao lao lilikuwa la offside.

Licha ya mpira kumalizika mashabiki hao wa Iran waliendelea kushangilia nje ya uwanja, huku wakisisitiza kwamba waliwamudu ipasavyo Hispania.