Sweden, Denmark ni utamu kunoga

SI unajua Sweden na Denmark zote zipo kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Russia? Denmark ipo Kundi C wakati Sweden imepangwa Kundi F.

Kwa hali ya mambo ilivyo, itakuwa ngumu kweli kweli kwa timu hizo kukutana katika raundi hizi za awali labda hapo itakapofika fainali.

Unajua, zitakapokutana kitu gani kitatokea? Kwanza habari zetu. Pili, Sweden na Denmark zinapokutana kwenye mechi zinazoandaliwa na Fifa, huwa zinatambulika kwa vifupisho, SWE vs DEN. Maneno hayo ukiyaunganisha unapata neno SWEDEN. Hapo utakuwa umeitaja nchi moja.

Lakini, maneno yaliyoachwa na Fifa kuhusu nchi hizo ni DEN kwenye SWEDEN na MARK kwenye DENMARK. Kwa maana hiyo, ukiunganisha majina ya DEN na MARK, ambayo yameachwa unapata neno DENMARK.

Hapo utakuwa umeitaja nchi ya pili. Huo ndio utamu wa kuhusu mechi za Sweden na Denmark zinapokutana kwenye mechi za fainali za Kombe la Dunia au zile zinazoandaliwa na Fifa kama vile za kirafiki.