#WC2018: Mambo ni Bayern na Inter Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Baada ya Croatia kutinga fainali ya Kombe la Dunia 2018 kwa kuwachaoa England, hiyo ina maana kwamba klabu hizo mbili, Bayern na Inter zimekuwa na wachezaji kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1982.

MOSCOW, RUSSIA. BAYERN Munich na Inter Milan pengine hazibeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda sasa, lakini miamba hiyo ya Ulaya imeonyesha kuwa na rekodi tamu kwenye Kombe la Dunia.
Baada ya Croatia kutinga fainali ya Kombe la Dunia 2018 kwa kuwachaoa England, hiyo ina maana kwamba klabu hizo mbili, Bayern na Inter zimekuwa na wachezaji kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1982.

Ivan Perisic na Marcelo Brozovic wote wanachezea Inter na watakuwapo kwenye mechi hiyo itakayopigwa Jumapili dhidi ya Ufaransa, ambayo itakuwa na huduma ya kiungo, Corentin Tolisso, anayechezea Bayern Munich. Cheki mastaa wa Bayern na Inter walivyotesa mechi za fainali Kombe la Dunia tangu mwaka 1982 hadi sasa 2018. Mastaa wao hawajakosa fainali.
1982 -Italia 3-1 Ujerumani Magharibi: Gabriele Oriali, Giuseppe Bergomi (Inter), Wolfgang Dremmler, Karl-Heinze Rummenigge, Paul Breitner (Bayern)
1986 - Argentina 3-2 Ujerumani Masharibi: Karl-Heinz Rummenigge (Inter), Norbert Eder, Dieter Hoeness, Lothar Matthaus (Bayern)
1990 - Ujerumani Magharibi 1-0 Argentina: Andreas Brehme, Jurgen Klinsmann, Lothar Matthaus (Inter), Stefan Reuter, Jurgen Kohler, Klaus Augenthaler (Bayern)
1994 - Brazil 0-0 Italia (Brazil ilishinda penalti 3-2): Nicola Berti (Inter), Jorginho (Bayern)
1998 - Brazil 0-3 Ufaransa: Youri Djorkaeff, Ronaldo (Inter), Bixente Lizarazu (Bayern)
2002 - Ujerumani 0-2 Brazil: Ronaldo (Inter), Jens Jeremies, Thomas Linke, Oliver Khan (Bayern)
2006 - Italia 1-1 Ufaransa (Itali ilishinda penalti 5-3): Marco Materazzi, Fabio Grosso (Inter), Willy Sagnol (Bayern)
2010 - Uholanzi 0-1 Hispania: Wesley Sneijder (Inter), Mark van Bommel, Arjen Robben (Bayern)
2014 - Ujerumani 1-0 Argentina: Rodrigo Palacio (Inter), Manuel Neuer, Philipp Lahm, Jerome Boateng, Bastian Schweinsteiger, Thomas Muller, Toni Kroos, Mario Gotze (Bayern).