Nataka kuona vijana wakitikisa Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Ligi hizo shughuli zilitamatika wikendi iliyopita. Sasa ndugu zanguni macho duniani zinaangazia vikosi vya nchi zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Rusia. Ni nchi 32 ambazo zinashiriki fainali hizo. Presha inazidi kufuata wachezaji ambao kila mchezaji anatazama kuitwa katika kikosi cha nchii yake.

Ligi Kuu Hispania, England, Ufaransa, Ujerumani na kadhalika zimefikia kikomo.

Ligi hizo shughuli zilitamatika wikendi iliyopita. Sasa ndugu zanguni macho duniani zinaangazia vikosi vya nchi zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Rusia. Ni nchi 32 ambazo zinashiriki fainali hizo. Presha inazidi kufuata wachezaji ambao kila mchezaji anatazama kuitwa katika kikosi cha nchii yake.

Kila mchezaji ameshikwa na dukuduku akitarajia kuhitimisha malengo ya kocha wa timu za kimataifa ya nchi yake. Ni nani atakaye chaguliwa?

Kuanzia wiki ijayo tutajaribu kuangalia kwa undani wa vikosi hivyo ni yupi alichaguliwa na hakustahili kuwepo katika kikosi hicho na ni yupi aliachwa nje na alistahili kuwepo katika kikosi cha nchi yake.

Hata hivyo, leo naingia ndani ya vikosi kadhaa na haswa madhumuni yangu ni kuchambua chipukizi ambao wametajwa katika vikosi hivyo. Chipukizi ambao natarajia kuona wakifanya mambo ya kiukweli katika kombe la dunia.

Andre Silva .. kinda wa timu ya taifa ya Ureno ni mchezaji ambaye anatarajiwa kuvaa viatu vya nahodha wao Cristiano Ronaldo. Itakuwa ngumu sana kupata mchezaji ambaye anaweza kuvaa viatu vya Ronaldo lakini kinda huyu natarajia anaweza kuvaa viatu hivyo.

Kinda huyu baada ya kuonyesha viwango vyake katika mashindano ya chipukizi wasio zidi miaka 20 nchini New Zealand na kufunga mabao manne anabakia mojawapo ya chipukizi ambao watu wengi wanatarajia kumuona akitesa pale Russia.

Andre Silva- chipukizi anayekichapa katika Ligi Kuu Italia akichezea klabu ya AC Milan atakuwa mojawapo ya wachezaji chipukizi ambao dunia itakuwa inaangazia. Anatazamiwa kuvaa vyatu vya Ronaldo wakati atakapo amua kustaafu.

Jee atapata nafasi hiyo kweli? Ni muda tu unasubiriwa.

Msimu ambao umepita tu kinda huyo amepachika mabao 34 jambo ambalo linamuweka katika ramani ya wanasoka wachanga duniani.

Kinda mwingine ambaye kwa kweli anatisha ndugu zangu ni Gabriel Jesus. Huyu chipukizi kwa kweli ametesa kweli kweli katika angaa za soka England na barani Ulaya. Jesus ambaye anakichapa Man City anatarajiwa kufanya kweli katika kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil. Kikosi ambacho kiko na washambulizi kama Neymar, Paulinho na kadhalika itabidi ametia bidii. Hata hivyo, kulingana na viwango ambavyo ameonyesha Ligi Kuu England hadi kupachika mabao 13 ni viwango ambavyo kocha yeyote yule hawezi muacha nje.

Natarajia kuona akitesa katika anga za Russia mwezi ujao. Gabriel Jesus ambaye alisajiliwa na kocha Pep Guardiola msimu huu ameonyesha dalili zote za kurithi Neymar iwapo atastaafu mapema.

Kasi aliyo nayo huyo kijana achaa tu. Ni kasi ya kupimia mbali sana. Kijana mwenye umri wa miaka 22 natarajia kuwa atakuwa lulu katika kikosi hicho cha Brazil miaka za hivi karibuni.

Rodrigo Bentancur mwenye umri wa miaka 20 anayetesa katika timu ya taifa ya Uruguay na ni kiungo wa klabu ya Juventus Italia ni kinda mwingine ambaye natarajia kuona akitesa angaa za Russia mwezi ujao.

Kijana ambaye alizaliwa namo Juni 25,1977 ni kinda ambaye niko na uhakika kwamba ataweza kufanya kweli pale Russia.

Suarez anatarajiwa kupigiwa pasi za kiukweli na kinda huyu ambaye ameonyesha ukomavu katika sekta hiyo.

Kijana huyu aliyekuwa akikipiga katika klabu ya Boca Juniors kwa kweli shughuli zake zilionekana wakati aliposaidia kikosi chake cha chipukizi wasiozidi miaka 20 kumaliza katika nafasi ya nne katika Fainali za Kombe la Dunia pale New Zealand. Sijui kama viwango hivyo atazidi kuviendeleza katika Kombe la Dunia mwezi ujao.

Edson Alvez, kinda wa timu ya taifa ya Mexico ni mkabaji, anaye sakata soka lake katika klabu ya Liga MX Club America. Kinda huyu shughli zake zilionekana mapema tu wakati alipoitwa katika kikosi cha kwanza katika timu ya taifa ya Mexico hata kabla hajawakilisha Mexico katika mashindano ya timu za vijana wasiozidi miaka 20.

Julai 30, 2017 kinda huyu aliitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya Taifa ya Mexico katika mechi ya kirafiki dhidi ya Iceland.

Februari 8, 2018 kinda huyu alipata kucheza mechi yake ya kwanza kabisa dhidi ya Ice akiingia katika nafasi ya Jesus Molina katika dakika ya 60. Kufikia leo kinda huyo amekipiga mara tisa katika timu ya Taifa. Ninatarajia kumuona akiendeleza shughuli hiyo hiyo vilivyo mwezi ujao.

Ni chipukizi wengi tuu ambao natarajia kuona katika vikosi hivi bila kumsahau Marcus Rashford wa Manchester Utd chipukizi ambaye pia ameitwa katika kikosi cha England kinachoongozwa na washambualiji, Harry Kane na Delle Ali. Chipukizi Lingard vile vile wa kikosi cha Manchester Utd natarajia kuona wakifanya mambo pale Russia baada ya wakongwe Wayne Rooney Wazza na Walcott kutemwa katika kikosi hicho cha Gareth Southgate.