STRAIKA WA MWANASPOTI: Nani mwenye ubavu wa kuwazuia Man City?

Tuesday February 13 2018Boniface Ambani

Boniface Ambani 

By Boniface Ambani, Nairobi

NINACHUKUA hii fursa kuwapa pongezi mabingwa Ligi Kuu England msimu 2017-18 Club ya Man City.

Kwangu kwa kweli hao tayari wanangojea tu kutawazwa ubingwa. Iwapo kuna mtu anapinga sijui ni nani lakini kufikia sasa hivi na alama ambazo wamezizoa, kwa kweli inahitaji miujiza kubwa sana klabu nyingine yoyote ile kutwaa ubingwa huo msimu hu.

Kocha Pep Guardiola katika msimu wake wa pili katika ligi hiyo, ameonyesha kila sababu ya

kutwaa ubingwa huo. Itakuwa vigumu kupoteza taji hilo.

Hebu angalia tangu msimu uanze, Pep na kikosi chake cha Manchester City wamepoteza mechi moja tu, mechi ambayo walipoteza ndani ya uga wa Anfield mikononi mwa klabu ya Liverpool.

Man City wameandikisha alama

72 ndani ya mechi 27 ambazo wamezicheza kufikia sasa.

Klabu ambayo inawafata kwa karibu ni Man Utd wakiwa na alama 56 tofauti ikiwa ni alama 16.

Liverpool ikiwafuata kwa karibu na alama 54.

Tottenham alama 52, Chelsea ikifunga ukurasa wa tano bora ikiwa na alama 50.

Manchester City ilitangaza ubabe wake wikendi iliyopita baada ya kuipiga Leicester City kichapo cha mbwa mwizi. Kichapo hiki, wengi hawakutarajia haswa wapenzi wa soka ambao

wanakifahamu kikosi cha Leicester City.

Mchezaji, Kun Aguero alipiga mabao manne pekee yake ndani ya hiyo mechi.

Kwa kweli ukiangali soka ambalo Man City wanalicheza ndugu zanguni hamna sababu ya kufikiria kuwa watalipoteza hilo taji msimu huu.

Wachezaji wake wote wamekamilika ndugu zanguni.

Katika kila nafasi ya mchezo, kuna zaidi ya wachezaji wawili wakali.

Leroy Sane, Fernadinho, Kun Aguero, Kompany, Raheem Sterling, ndugu zanguni hao ni baadhi tu ya wachezaji ambao bila shaka huwezi kukosa la kufanya nao.

Ni wachezaji wakiwa ndani ya kikosi chako hakuna kutishwa na klabu yoyote ile.

Taji hilo lilikwenda kwa Man City hii wikendi wakati Manchester Utd walipoteza mechi yao Jumapili dhidi ya Newcastle. Manchester Utd walikuwa na matumaini ya kuwafukuzia Man City lakini kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Newcastle basi mambo yaliwaendea mrama.

Kilichobakia kati ya Man Utd, Chelsea, Liverpoool, Totteham na Arsenali ni kupigania nafasi ya kuingia ndani ya nne bora angalau msimu ujao wajikatie tiketi ya kuwakilisha England katika Ligi Mabingwa Ulaya.

Manchester United nayo pia imeendelea kuandikisha matokeo ambayo hayaridhishi kabisa hata baada ya kumsajili nyota wa klabu ya Arsenal, Sanchez.

Kupoteza mechi dhidi ya Newcastle kwa kweli iliwaacha katika nafasi ya pili ikiwa wako mbali kwa wapinzani wao na mahasidi wao wa tangu jadoi Man City.

Shida kubwa ya Manchester Utd ni safu yao ya ulinzi. Mabeki wamekuwa na shida kubwa tangu kuondoka kwa Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra katika hiyo safu mambo hayajakuwa sawa hadi leo.

Kumekuwa na shida kubwa katika safu hiyo. Sijui Jose The Special one atafanya jambo gani kuimarisha ngome hiyo. Masaibu yanayo mkumba

Jose katika safu ya ulinzi ni masahibu ambayo pia kocha Arsene Wenger anapitia ndugu zanguni.

Klabu hizo mbili, zimeshindwa kabisa kusajili wachezaji wa kujaza nafasi zilizioachwa na mababe wa klabu hzo takriban miaka mitano iliyopita.

Matumaini ya klabu ya Arsenali kumaliza katika nafasi ya nne bora yalizidi kudidimia baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao wa tangu jadi klabu ya Tottenham.

Bao ambalo lilifungwa na Kane katika dakika ya 49 kipindi cha lala salama ndilo bao ambalo lili katisha Arsenali tama ya kumaliza ndani ya nne bora msimu huu. Arsenali wamo katika nafasi ya sita wakiwa na alama 45.

Ni nafasi ambayo kwa kweli wapenzi wa soka haswa mashabiki wa Arsenali hawafurahii.

Manchester Unites walikuwa wakiitawala nafasi hiyo kitambo.

Hamna la kufanya lakini kuzidi kupambana na hali yao wenyewe.