Naipa nafasi Senegal hutua ya pili

Muktasari:

  • Ni imani yangu siku moja nitapata nafasi ya kuishuhudia Tanzania ikishiriki katika Kombe la Dunia lakini hata sasa napenda sana kufuatilia timu zote za Afrika zinazoshiriki katika fainali hizo kwa kuwa pia wanawakilisha bara letu la Afrika.

FAINALI za Kombe la Dunia zimebakisha siku moja tu kutimua vumbi.

zinakaribia kwa kasi sana na bila shaka mashabiki wote wa soka wanazisubiri kwa hamu kuona timu bora zaidi duniani zikipambana katika michuano mikubwa zaidi duniani.

Ni imani yangu siku moja nitapata nafasi ya kuishuhudia Tanzania ikishiriki katika Kombe la Dunia lakini hata sasa napenda sana kufuatilia timu zote za Afrika zinazoshiriki katika fainali hizo kwa kuwa pia wanawakilisha bara letu la Afrika.

Naamini mashabiki wote wa soka Afrika walifurahi sana mwaka 2010, Ghana ilipofikia robo fainali ya Kombe la Dunia. Naamini mwaka huu Afrika inawakilishwa na timu zenye viwango vya juu kama Misri, Tunisia, Nigeria, Senegal na Morocco. Lakini, kati ya timu hizi ni imani yangu Senegal ni timu yenye nafasi kubwa zaidi

kuvuka hatua ya makundi na huenda kufika hata mbali zaidi katika Kombe la Dunia.

Senegal hivi sasa ina kikosi chenye wachezaji wengi chipukizi pamoja na wachezaji ambao wana uzoefu mkubwa wa kucheza Ulaya.

Bila shaka matumaini ya Wasenegali yapo katika mabega

ya mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane.

Katika timu ya Liverpool mchezaji huyu ni winga lakini katika Timu ya Taifa ya Senegal nafasi ya Sadio Mane mara nyingi inamruhusu kucheza pia kama namba kumi na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao kwa wachezaji

wenzake.

Ingawa Senegal inamtegemea sana Sadio Mane nguvu ya timu hiyo ni kwamba kuna wachezaji wengine wenye viwango vya juu nyuma yake. Katika kundi la Senegal kuna timu yenye uwezo mkubwa wa kucheza mpira wa kushambulia kama Colombia na Poland lakini beki wa kati wa Senegal, Koulbally, ambaye anacheza Napoli ana kiwango cha kidunia na hivyo ngome ya Senegal ipo imara sana. Pia, timu hiyo ina uwezo wa kufunga mabao hata kama haimiliki mpira kwa muda mrefu kwa kuwa wachezaji kama Diao Balde Keita na Sadio Mane wana kasi sana na uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza.

Nikiitazama Senegal kuna shida moja tu katika timu hiyo na haina viungo wenye uwezo mkubwa wa kutoa pasi za mbali na kuongoza mchezo.

Idrissa Gueye ambaye anachezea Everton, Bado Ndiaye wa Stoke na Chaikhou Kouyate wa Westham wote ni viungo wenye viwango vya juu lakini wote ni viungo wakabaji na nguvu yao ipo katika uwezo wao wa kusoma mchezo na kukaba lakini sio katika kutoa pasi.

Hata hivyo, naamini kama Kocha wa Senegal, Aliou Cisse, atafanikiwa kutumia mfumo ambao utamruhusu Sadio Mane kucheza kama namba kumi, basi Senegal itakuwa na mchezaji wa kutoa pasi za mwisho na kuanzisha mashambulizi hata kama viungo wao ni viungo wakabaji zaidi.