MO ajihadhari na kisa cha mambo ya fedha hisa za Simba

Muktasari:

Ndani ya albamu hii kulikuwa na wimbo ulioitwa “Mambo ya fedha” alioimba kwa kumshirikisha chipukizi wa wakati huo, Lady Jay Dee, ambaye alikipamba vilivyo kiitikio.

KATIKA kuikaribisha karne mpya ya 21, mwimbaji wa BongoFlava Mr. II a.k.a Sugu, alikuja na albamu iliyoitwa Millenium.

Ndani ya albamu hii kulikuwa na wimbo ulioitwa “Mambo ya fedha” alioimba kwa kumshirikisha chipukizi wa wakati huo, Lady Jay Dee, ambaye alikipamba vilivyo kiitikio.

‘Fanya unachoweza (Mambo ya Fedha) Sema unachoweza (Fedha)

Mbona unashangaa....mambo ya fedha)’

Ubeti wa kwanza wa ‘ngoma’ hiyo, Sugu alisikika kama akitoa lawama kwa mtu wake wa karibu kuhusu mambo ya maslahi...

‘Unaponiangalia usoni nini unachokiona?

Nimeshapitia matatizo mengi ya kila aina...Mbona tunagombana!

Familia yako na yangu wote tunajuana

Na zaidi sisi sote bado vijana

Tunaweza kutekeleza kile tunachoweza

Kwenye mambo ya fedha.’

Stori zilizokuwepo wakati ule ni kwamba, Sugu alikuwa akitoa ujumbe kwa jamaa yake wa karibu aliyekuwa na makubaliano naye ya kibiashara kwa ajili ya kusambaza albamu yake ya pili ya NDANI YA BONGO iliyotoka 1996/97.

Ilisemekana kwamba, jamaa aliiona fursa kwa Sugu na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla, akavutiwa kuwekeza.

Albamu ya kwanza ya Sugu ‘Ni Mimi’, iliyotoka 1995/96, haikuuza sana sokoni kutokana na ugeni wa muziki wa Hip Hop na Rap. Lakini licha ya kusuasua sokoni, albamu hiyo ilichangia sana kuutambulisha zaidi muziki huu kwa watu wa kada mbalimbali, tofauti na hapo kabla. Hii ilitengeneza njia kwa albamu zilizokuwa zikifuata, ikiwemo hii ya Ndani ya Bongo, kuuzika sokoni. Kwa hiyo, kwa watu wenye jicho la kuona fursa kama jamaa wa Sugu, hili lilikuwa dili.

Japo haikuwahi kuthibitishwa na yeyote, lakini duru za wajuzi wa mambo zilisema kwamba wakati Sugu akikamilisha kurekodi albamu ya Ndani ya Bongo, alikubaliana na jamaa kwamba itakapotoka, atasimamia majukumu yote ya usambazaji na uuzaji nchi nzima. Jamaa aliandaa mpango wa kibiashara ikiwemo promosheni ya mtaa kwa mtaa kwa sababu wakati huo hakukuwa na redio iliyotaka kupiga hewani ‘uhuni’. Kwa kifupi, jamaa akawekeza kisawasawa!

Lakini kwa mshangao wa wengi, taarifa zilidai kwamba albamu ilipokamilika, Sugu akamtosa jamaa baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa wadosi wa GMC. Jamaa akakonda moyo, bifu likazuka. Sugu akahama nchini na kwenda Uholanzi (sio kwa kumkimbia jamaa lakini) ambako alifanikiwa kutoa albamu moja ya Nje ya Bongo.

‘Maisha kurekebisha unataka’ kuleta zako zipiMaisha yenyewe ni mafupi, Nje ya Bongo...’

Hiki kilikuwa kiitikio cha wimbo uliobeba jina la albamu, Nje ya Bongo, ambacho kwa asilimia kubwa kilipita kwenye njia ile ile ya Ndani ya Bongo huku kikimchana jamaa kimtindo.

Jamaa akabaki nchini na kuandaa ‘project’ zingine kwa kuwekeza kwa waimbaji wengine. Kubwa kuliko zote, akawa bosi kwenye taasisi moja iliyojikita katika muziki hasa wa kizazi kipya.

Kwa hiyo Sugu aliporudi Ndani ya Bongo akitokea Nje ya Bongo mwaka 2000, alimkuta jamaa bado ana kinyongo naye na mbaya zaidi, kaushika muziki wa Tanzania kupitia ile taasisi na zile project zake.

Ikabidi Sugu afunguke kutaka suluhu kimistari kumwambia jamaa kwamba alichokifanya wakati ule kilisababishwa na “Mambo ya fedha” na isitoshe kwa

umri wao bado wana safari ndefu ya kuzisaka fedha. Kwa hiyo hakukuwa na haja ya kumaindiana...achukulie poa tu!

Lakini jamaa kama binadamu wa kawaida, asingeweza kuchukulia poa hasara aliyopata kwa kuuwekeza mawazo, fedha na muda, halafu akaambulia

patupu...lakini mwisho wa siku, jamaa aklifungua njia lakini wakapita watu wengine kabisa!Haikuwahi kuthibishwa wakati ule mpaka wakati huu, lakini hata hivyo, mkasa wa Sugu na jamaa yake, unafanana na ule wa bwana mmoja wa kuitwa Greg Dyke na kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya England, EPL 1992.

Mfumo wa zamani wa soka la England, ulioanza 1888, ulikuwa wa madaraja manne; Daraja la Kwanza hadi la Nne. Mfumo huu uliitwa English Football League na ulisimamiwa moja kwa moja na Bodi ya Ligi ya English Football League kwa idhini ya Chama cha Soka nchini humo, FA. Daraja la kwanza nd’o

ilikiwa ngazi ya juu zaidi.

Mfumo huu uliendelea mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1990 pale Mkurugenzi wa Kituo cha Televisheni cha ITV kupitia matangazo ya mwisho wa wiki jijini London (London Weekend Television (LWT)), Greg Dyke alipoona fursa ya kibiashara kupitia soka. Akaandaa ‘dina’ kwa wawakilishi wa klabu tano kubwa kwa wakati huo; Arsenal, Everton, Liverpool, Manchester United na Tottenham Hotspur ili kuyajenga. Mkutano huo ulifanyika 1990. Kupitia mkutano huo wa ‘dina’, Greg Dyke alivishawishi klabu hizo kujitenga na Football League na kuanzisha ligi yao (ilipendekezwa iitwe English Super League) ili kujipatia vipato vikubwa zaidi kutokana na mgao wa haki za matangazo ya luninga ambayo kwa wakati huo yalikuwa yakigawanywa kwa timu zote kuanzia Daraja la Kwanza mpaka la Nne. Dyke alizieleza klabu hizo kwamba zikijitenga, mapato yote yatakuwa ya kwao peke yao.

Lengo la Dyke lilikuwa kununua haki za matangazo hayo (kupitia kituo chake) pale mpango wa kujitenga utakapokamilika.

Klabu zikamuelewa Dyke na kuanzisha uasi kwa Football League na FA kwa ujumla zikitaka kujitenga. Haikuwa habari njema kwa FA kwa hiyo ikapinga kwa nguvu zote ikihofia kupoteza haki zake katika ligi ambayo waliianzisha na kuiendesha kwa zaidi ya karne moja.

Kwa ushauri wa Dyke, mgogoro ukafika Mahakama Kuu na mwaka 1991 mahakama ikaamua kwamba klabu zina haki ya kujitenga. Uamuzi wa kihistoria zaidi ya uamuzi wa mahakama ya Kenya, ulitolewa na Jaji Justice Rose. Klabu za Daraja la Kwanza zikajitenga na kuanzisha FA Premier League mwaka 1992 ambayo baadaye ikabadilika na kuwa English Premier League EPL.

Baada ya mpango wa kujitenga kufanikiwa, ikatangazwa tenda ya kununua haki za matangazo ya luninga, cha kushangaza, Greg Dyke na ITV yake wakapigwa bao na kituo cha TV cha BSkyB, kilichokatoa donge nono la £304m na kushinda tenda kwa mkataba wa miaka mitano.

Licha ya kuwekeza muda, mawazo na fedha, Greg Dyke na ITV, wakaambulia patupu.MO Dewji na Hisa nza Simba

Simba SC inaelekea kwenye zama mpya za uendeshaji kwa kukaribia kuanza kuuza hisa kwa wanachama wake.

Kama ilivyokuwa kwa Sugu na jamaa yake au klabu za England na Dyke, nyuma ya mpango huu wa Simba, yupo mfanyabiashara tajiri kijana anayetoka kwenye familia ya Simba lialia, Mohammed ‘MO’ Dewji. Yeye ndiye ‘aliyetekenya’ hisia za mashabiki wa Simba wakati akiongea na kipindi cha Mkasi TV cha Eatv. “Nimeongea na Rais wa Simba na ameniambia nimwandikie paper. Unajua mimi nimemwambia ‘wewe unafikiria mimi nikinunua hisa 51% ya Simba, maana yake nitaipeleka wapi?’ Mimi ni mtu wa hapa hapa na naipenda Simba. Leo mashabiki wa Manchester United, Arsenal they don’t care klabu ya nani, wanachohitaji ni mafanikio. Mimi nimewaambia nipo tayari niwekeze bilioni 20. Leo Katumbi wa TP Mazembe ni timu yake na inafanya vizuri. Mimi nimewaambia hata nikiwekeza bilioni 20 sitaona hela, mimi na biashara mia nyingine ninapata hela.”

Hapo MO akawatia wazimu watu wa Simba na wao wakautia presha uongozi. Hali ya hewa ikachafuka. Mara zote timu ikifanya vibaya, mashabiki wanalia na viongozi wampe timu MO.

MO mwenyewe hakubaki nyuma, aliendelea kushinikiza chini kwa chini kupitia mahojiano mbalimbali aliyoyafanya na vyombo vya habari.

Kuonesha utayari wake, Mo ‘aliusogeza’ karibu yake uongozi na kuutatulia matatizo madogomadogo. Lakini alikuwa mjanja kuhakikisha anaweka ushahidi kila anapofanya jambo kuisaidia timu hiyo. Kwa mfano, alipotoa Shilingi 100 milioni za usajili wa Mavugo, alifanya hivyo mbele ya kamera za waandishi.

MO amepitia mengi ya kukatisha tamaa katika harakati za kuleta mabadiliko Msimbazi. Mawazo yake ndiyo yaliyowafumbua macho wanachama na

kulazimisha mfumo mpya na sasa mchakato umefikia pazuri na tayari kamati ya kusimamia mchakato mzima.