Kwa ubora upi Messi asiwepo!

Muktasari:

Wakali wote hao ni wa viwango vya juu. Messi ambaye jina lake halimo, pengine ni bora zaidi yao. Ni bora zaidi yao. Pengine hilo ndilo lililowafanya Fifa wasimshindanishe awamu hii. Hakuna anayepaswa kushindana naye.

MZUKA umepungua. Tuzo ya Fifa ya mchezaji bora wa mwaka, imepungua kidogo utamu wake tofauti na wakati ile ilipokuwa ikitolewa kwa pamoja na Ballon d’Or.

Kwa sasa tuzo hizo zimekuwa mbinu tofauti, hakika zimepoteza ule utamu wake.

Lakini, zaidi ya yote, tuzo ni tuzo. Waliotinga tatu bora ya safari hii kwenye tuzo hizo za Fifa, jina la Lionel Messi halipo.

Wachezaji watatu wa safari hii watakaowania tuzo hiyo ya Fifa ni Cristiano Ronaldo, Mohamed Salah na Luka Modric.

Wakali wote hao ni wa viwango vya juu. Messi ambaye jina lake halimo, pengine ni bora zaidi yao. Ni bora zaidi yao. Pengine hilo ndilo lililowafanya Fifa wasimshindanishe awamu hii. Hakuna anayepaswa kushindana naye.

Kwa rekodi za mwaka mmoja uliopita, Messi ameshinda La Liga, ameibeba Argentina kwenye Kombe la Dunia na kukomea kwenye hatua ya 16 bora, Nadhani alibeba pia tuzo ya ufungaji bora kwenye La Liga msimu uliopita. Kwenye orodha hayumo. Mo Salah hakushinda taji lolote kwa mwaka wote uliopita, ameshinda tuzo ya mfungaji bora kwenye Ligi Kuu England, lakini klabu yake ya Liverpool ilikamata nafasi ya nne kwenye ligi na ilichapwa kwenye fainali ya Uefa.

Timu yake ya taifa ya Misri aliyoisaidia kufuzu Kombe la Dunia imekomea hatua ya makundi na haikushinda mechi yoyote. Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alicheza kwa dakika chache tu, lakini yumo kwenye tuzo ya Fifa.

Ronaldo yumo kwenye tuzo hiyo kutokana na kubebwa na rekodi zake kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, akibeba taji akiwa na aMadrid. Modric amebeba taji la Uefa na amefika fainali na Croatia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa fainali hizo. Kwenye orodha hiyo ya Fifa, kiungo huyo ndiye anayeonekana kuwa na kitu kinachostahili kupewa tuzo.

Lakini, kwa hao wengine wote hakuna aliyefanya kitu cha ajabu kuzidi mafanikio ya Muargentina huyo. Pengine Fifa imeamua kutufungua macho kwamba Messi hakuna anayestahili kushindanishwa nao.

Timu ya Salah iliachwa pointi kibao na Man City kwenye Ligi Kuu England. Timu ya Ronaldo iliachwa pointi 17 na timu ya Messi kwenye La Liga. Ronaldo na Modric wote waliteswa na Messi kwenye michuano ya ndani, ubora huo unatokea wapi.

Kwenye michuano ya Fifa, Messi amepoteza kwa Ufaransa, waliokuja kuwa mabingwa, Ronaldo amepoteza kwa Luis Suarez.

Mechi iliyopita tu hapo, Messi kapiga bao mbili na kuasisti nyingine mbili, lakini Ronaldo amecheza dakika 270 kwenye Serie A bila ya bao wala asisti. Ubora upi.