Kilimanjaro Stars ukweli imetia aibu Chalenji

Muktasari:

Katika Kundi la A, ambalo linajumuisha Uganda, Burundi, Ethiopia, Zimbabwe na Sudan Kusini ingawaje Zimbabwe haikufika, Uganda na Burundi na Ethiopia ziko na matumaini makubwa ya kusonga katika nusu fainali.

MASHINDANO ya kuwania taji la CECAFA yanazidi kunoga na kuzidi kukaribia hatua za nusu fainali.

Ni wazi kufikia sasa hivi ni nchi gani zinaonekana zikiwa na uwezo mkubwa wa kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika Kundi la A, ambalo linajumuisha Uganda, Burundi, Ethiopia, Zimbabwe na Sudan Kusini ingawaje Zimbabwe haikufika, Uganda na Burundi na Ethiopia ziko na matumaini makubwa ya kusonga katika nusu fainali.

Wakati ninaingia mitamboni Uganda walikuwa wanaongoza jedwali hilo wakifuatiwa Kwa karibu na nchii ya Burundi.

Uganda Cranes ni mojawapo ya nchii ambazao zinapigiwa upato wa kushinda taji hilo mwaka huu.

Katika Kundi la B kuna wenyeji Kenya,Zanzibar, Tanzania,Libya na Rwanda.

Cha kushangaza kabisa ni kwamba nchi ambayo haikutarajiwa kufanya vyema katika mashindano hayo, Zanzibar inaongoza Kundi A ikiwa na alama saba ikifuatiwa na Kenya ambayo iko na alama tano Rwanda alama nne,Libya alama 3, Tanzania Bara ikishikilia mkia katika jedwali hilo na alama moja.

(Hii ni kabla ya mechi za jana)

Nikiingia mitamboni Tanzania Bara walikuwa wanajitayarisha kupiga mechi yao ya mwisho na Harambee Stars.

Swali langu leo ni mbona Kilimanjaro Stars soka lao limeshuka hivyo?

Ukiangalia kwa ndani ndugu zangu Watanzania ni wazi kuwa soka la Tanzania linazidi kushuka kwa viwango jambo linalofanya soka la Tanzania kushuka kwa viwango la kwanza ni wakati shirikisho la soka Tanzania lilinzisha mfumo wa usajali wa wanasoka wa kigeni. Walipunguza kabisa idadi ya wachezaji ambao wanafaa kusajiliwa.

Ukiangalia nchi ambazo zimeendelea kisoka hawana vikwazo vya usajili. Hawa wachezaji huwa ni changa moto kwa wachezaji wazawa.

Enzi tulikuwa Yanga miaka kama sita iliyopita wakati huo, hakika soka la Tanzania lilikuwa limeinuka vizuri saana.

Wachezaji was timu ya Taifa walikuwa na viwango vya juu saana. Kila Mchezaji alikuwa anajitolea afikie viwango vyetu.

No Jambo ambalo lilisaidia soka la Tanzania. La pili ni waandishi wa magezeti Tanzania. Wanawapa sofa nyingi saana wachezaji wa Tanzania.

Kila kukicha ni magazeti na sifa ambazo sio za kiukweli. Wakati umefika wa kusema ukweli. Hizi gazeti za Simba na Yanga ndugu zanguni zimekuwa zikiwapa wachezaji sifa hawastahili kupewa. Ni vyema kuwaambia wachezaji ukweli. Kuwalimbukizia sifa hakuna ni Jambo ambalo halifai.

Ni kubomoa wachezaji waambieni ukweli.

Magazeti hayo yanawafanya wachezaji hawa wa Tanzania kuwa mastaa bure tuu. Nikiangalia soka ambalo linachezwa na Tanzania Bara kwa kweli ni soka na kutia aibu ndugu zangu wa Tanzania.

Kuna baadhi ya wachezaji wamo katika kikosi hicho hawastahili kuwepo kabisa katika kikosi hicho. Matamshi ya kocha pia juzi yanamponda yeye mwenyewe. Kusema wachezaji hawakuwa fiti inamaanisha nini?

Ligi Kuu Tanzania ilianza kitambo. Na amechagua wachezaji kutoka hiyo hiyo ligi.

Itakuwaje aanze kusema kuwa wachezaji hawako fiti. Kwani aliona nini ndio akawaita kwenye kikosi.

Jambo la mwisho ndugu zanguni ni kwamba Wachezaji wetu wa Kitanzania wanaamini nguvu za giza sana.

Babu kama hajatembelewa inakuwa no balaa. Hizo vitu havipo katika soka kabisa. Soka ni lazima ufanye bidii. Mazoezi lazima uwe nayo ya kutosha.

Ni lazima tuu unitolee. Bila hivyo itakuwa ni hekaya za abunuasi kila wakati. Inatia aibu kubwa Kwa Tanzania Bara kufungwa na timu kama Zanzibar ndugu zanguni.

Na aibu, Zanzibar wanatinga hatua za nusu fainali Tanzania wakibebeshwa mizigo kurudi Dar. Shirikisho la Soka Tanzania TFF ni wakati wa kuchukua majukumu ya kurudisha soka Tanzania. Ni vyema kuweka mikakati za usajili ya wa wachezaji wa kigeni.

Ni lazima wachezaji wanao sajiliwa katika klabu zenu Tanzania wawe wanachezea timu zao za kitaifa.

Hiyo ni changamoto kwenu. Namba ya Sheria ya wachezaji wa kigeni wanaofaa kuchezeshwa katika klabu iondolewe. Hiyo tuu itasaidia wachezaji wa Tanzania kutia bidii.

Sifa magazetini Kwa wachezaji wenu ipunguzwe. Nimekuwa nikitazama hizo mechi na hao wachezaji wa Yanga na Simba ambao wamekuwa wakisifiwa magazetini sio lolote kwao.