STRAIKA WA MWANASPOTI: Kivumbi kikali cha ufungaji bora Ligi Kuu Kenya

Muktasari:

Katika Ligi Kuu msimu huu, mastraika wetu wamezembea kazini si kama hapo awali ambako kulikuwa na ushindani mkubwa sana.

Imesalia kama mechi tano Ligi Kuu ya Kenya kukamilika na mechi saba kuhitimisha Ligi ya Daraja la Pili almaarufu ‘National Super League’. Katika Ligi Kuu msimu huu, mastraika wetu wamezembea kazini si kama hapo awali ambako kulikuwa na ushindani mkubwa sana.

Hili lilikuwa tuzo ambalo kila mshambulizi alikuwa analimezea mate, lakini wakati huu tumeshindwa kuelewa tatizo liko wapi haswa. Je ni mabeki na makipa ndio wanaotia fora kutekeleza jukumu yao ama ni washambulizi ndio wamezembea uwanjani.

Kufikia sasa, kwenye jedwali la wanaoongoza kwa ufungaji bora utastaajabu kwa kuwa anayeo ngoza ni mchezaji aliyesajiliwa kwenye awamu ya pili ila kuna wachezaji ambao, wamekuwepo pindi ligi ilipoaanza na wamepitwa.

Jameni hili ni janga kuu ambalo linafaa kuangaziwa kwa undani haswa kwa wachezaji wa hapa kwetu nyumbani kenya. Matarajio ya mchezaji wa nchi ya kigeni kunyakua taji hili mara ya kwanza baada ya Danny Sserunkuma inaanza kuonekana.

Hii ni kwa sababu aliyekuwa anaoongoza ambaye ni Stephen Waruru wa Ulinzi Stars akiwa na jumla ya mabao 11 alikosa kumakinika kidogo, kilichomfanya Umaru Kasumba na Medddie Kagere wa Gor Mahia kumfikia.

Kepha Aswani, ambaye pia yupo kwenye mpambano huo na jumla ya mabao 10. Safari yake ilikumbwa na matatizo na timu yake Nakumatt FC ilikuwa imesimamishwa kucheza na pia alikuwa amesimamishwa kucheza kutokana na mkusanyiko wa kadi za njano kisa kilichomfanya kutocheza mechi kadhaa.

Jambo ambalo limekuwa changamoto kwake. Ushindano bado upo kwa kuwa kuna wachezaji ambao pia hawajawaachwa nyuma kwenye kivumbi hiki wachezaji ambayo wamecheka na nyavu mara tisa ni Jacques Tuysienge [Gor Mahia], Chrispin Odour [Mathare United], na wale wako na mabao manane ni Juma masoud wa kariobangi sharks na Ezekiel Okare wa sofapaka.

Hata hivyo, Kepha Aswani wikendi iliyopita alirejea kwenye ari yake na kupiga mabao mawili yaliyo msukumu kileleni mwa jedwali la wafungaji bora. Ikumbukwe ni baada pia ya mimi hapa kuwafokea kwenye mitandao ya jamii,jambo ambalo liliwapa changamoto na kuweza kuinuka.

Vile vile kwenye National Super League ambapo kila timu inatia bidi kufuzu kupanda daraja kuu. Kumekuwepo na ushindani mkubwa kwa ufungaji, kila mchezaji anatia bidii kuisaidia timu kwa kufunga mabao. Hadi sasa ni ngumu kubaini ni nani atakayeshinda taji hilo la ufungaji bora kutokana na kasi iliopo kwenye ligi hii.

Ni wachezaji sita ambao wameweza kufikisha mabao kumi na zaidi msimu huu. Anayeongoza kwenye jedwali ni mchezaji wa Vihiga United Patrick Okullo ambaye amefunga mabao 14 na kuna uwezekano anaweza kumpiku Mike Madoya wa Kericho Zoo ambaye alikuwa mfungaji bora msimu uliopita na jumla ya mabao ishirini. Patrick ndio kiini cha vihiga kutawala kwenye ligi licha ya mabao anazozifunga ni mchezaji anayecheza kwenye kiungo cha kati.

Mchezaji anayeshikilia nafasi ya pili ni kwa ufungaji bora ni Benson Amianda ambaye amefunga mabao k12.

Amianda akishirikiana na mchezaji mwenzake Lwamba Bebeto ambaye naye amefunga magoli manane wamesaidia timu yao ya Ushuru kuwa na matumaini ya kurejea kwenye Ligi Kuu.

Wachezaji ambao pia wako kwenye kivumbi hiki ni Erick Kapaito [Talanta FC], Pitson Mutamba [wazito] na Simon Abuko [KCB] ambao kila mmoja amefunga magoli 11.

Licha ya timu ya talanta kutofanya vizuri msimu huu, jambo hili halijamzuia Erick Kapaito kucheka na nyavu kumfanya kwa mchezaji ambaye amefunga magoli zote bila penalty. Wazito nao wanamtegemea mshambulizi wao Mutamba, ambaye yupo na magoli zaidi kuliko washambulizi mwenza Austine Ochieng na Joseph Waithira wakiwa na magoli matano kila mmoja.

Kulingana na hali hii tunaweza kuona kuna vile mastraika kwenye Ligi Kuu wamelala kazini.

Ni jambo la kustaajabisha kuona wachezaji wanajituma na kutekeleza majukumu zao vyema kuliko wale ambao wanaocheza Ligi Kuu.

Ukosefu huu wa mabao kwenye ligi kuu umevuka mpaka hadi kwenye timu yetu ya taifa.

Swali la kujiuliza hapa ni kwanini washambuliaji hawafungi mabao wakati utamu wa soka ni mabao na nina uhakika hakuna shabiki anayefurahia kwenda kulipa kiingilia uwanjani kuona mechi isiyokuwa na mabao.

Ni changamoto kubwa saana kwa mastraika wetu wanafaa kumakinika na kutia fora na kutupea sisi mashabiki haki yetu ambayo ni kutazama wakicheka na nyavu. Ninapohitimisha maoni yangu kutokana na jambo hili tatizo kubwa kwa washambulizi wetu ni ukosefu wa mpito na msimamo wa kucheza kuanzia utotoni hadi kwenye Ligi Kuu.

Hatuna washambulizi ambao wamekuwa katika hali nzuri ya kufunga kwa muda wa miaka zaidi ya tatu hivi tukimtoa Olunga na Were Jesee. Tukiangazia ulimwengu wa soka tunao wachezaji ambao, wanafunga mabao mengi kila msimu kama Messi, Ronaldo, Zlatan na Lukaku.

Hii inatokana na ile uzoefu na mpito ambao, mchezaji amepitia kuanzia kwenye taaluma zake za ujana wake. Ni wakati ambapo wakufunzi wetu wanafaa kuwatayarisha wachezaji kuanzia kwenye umri mdogo ndio wanapokuwa wakubwa itakuwa wana uzoefu na mpito ivyo basi tutaweza furahia kuona mechi inayokuwa na wingi wa mabao na hivyo ndivyo tutakavyo liinua soka letu nchini.

Kam ulitazama mechi ya Betis na Valencia basi huna budi kufurahia kuona vile mastraika walikuwa wana chambua makipa. Duh! Mechi iliishia 3-6 Betis wakiadhibiwa nyumbani kwao na Valencia. Raha mtupu.