Zari aweka mambo hadharani

Muktasari:

  • Si unajua kuna tetesi zinazoendelea mitandaoni kuwa Zari amerudiana kimapenzi na Diamond.

UNAAMBIWA ngoma bado mbichi mwanangu. Zari Thebosslady ameliamsha dude huko WCB.

Si unajua kuna tetesi zinazoendelea mitandaoni kuwa Zari amerudiana kimapenzi na Diamond.

Basi Zari amesafisha hali ya hewa kwa kuiweka sawa na kufafanua kilichopo ni makubaliano ya kushirikiana kama wazazi katika kuwalea watoto wao na si vinginevyo.

Kupitia mtandao wa SnapChart Zari aliandika:

“Katika kuweka mambo sawa, hatujarudiana lakini tumekubaliana kama wazazi jinsi ya kuwa wazazi bora kwa ajili ya watoto wetu wapendwa. Hii ni taarifa kwa mashabiki wetu. Tunawapenda sana.”

Hizi si taarifa nzuri kwa mashabiki waliokuwa wakivutia na wawili hao na kutamani kuwaona tena wakiwa pamoja.

Hivi karibuni meneja wa Diamond, Babu Tale alienda Afrika Kusini kwa Zari kujaribu kusuluhisha tofauti za wawili hao.

Hakuna yeyote kati yao aliyetoa jibu la uhakikika iwapo uhusiano huo umerudi zaidi ya hiki alichoeleza Zari.

Katika uhusiano wao Zari na Diamond walijaliwa kupata watoto wawili ambao ni Tiffah na Nillan.

Zari ndiye aliyetangaza kuvunja uhusiano wake na Diamond, Februari 14, mwaka huu ikiwa ni Siku ya Wapendanao baada ya kudai staa huyo alikuwa akimvunjia heshima kwenye mitandao kwa kuwa karibu na wanawake alioachana nao huku wakionyesha hisia za kimapenzi.