Zari awajibu mubashara wanaomsengenya Chibu wake

Muktasari:

Katika moja ya katuni ambayo imetengenezwa ikimuionyesha mfano wa Diamond na Zari, huku Zari akiwa anamvuta Diamond na Diamond akisema “Ni shetani kanipitia tu,” na pembeni kuna mfano wa shetani ambao unasema “Uongo niko nae

HUKU na huku Zari ni kama ameanza kujibu taratibu na kuweka wazi kuwa hali ni shwari kwa upande wa mapenzi yao ambayo karibuni yameingia doa.
Katika moja ya katuni ambayo imetengenezwa ikimuionyesha mfano wa Diamond na Zari, huku Zari akiwa anamvuta Diamond na Diamond akisema “Ni shetani kanipitia tu,” na pembeni kuna mfano wa shetani ambao unasema “Uongo niko nae,”.
Zari ameamua kujibu kwa kuandika “Wacha nirudishe akili yake, bye shetani,” ambapo amesababisha watu wengi kuachia maoni kutokana na maneno hayo.
Upande wa Hamisa Mobetto bado hajatia neno lolote mpaka sasa ambapo baadhi ya vyanzo vinasema kuanzia Jumatatu upande wa Hamisa umepanga kutoa tamko lao.