Zari aongea mazito amkumbuka mume wake Ivan Don

Muktasari:

Ivan Don, alizaliwa Desemba 12, 1977 katika mji wa Kayunga, Uganda, amefariki Mei 25, 2017, katika hopitali ya Steve Biko Academic iliyopo Pretoria, Afrika Kusini nakuzikwa kwao Uganda.

 Mwaka sasa tangu aliyekuwa mume wa Mfanyabiashara  Zarinah Hassan 'Zari', marehemu  Ivan Semwanga maarufu kwa jina la Ivan Don afariki dunia.

Lakini, wakati wanakumbuka siku hiyo ambayo ni leo Ijumaa, Zari amezungumza mengi  juu ya Ivan Don.

"Ni mwaka sasa tangu umetutoka, Mwenyezi Mungu amekuchukua lakini miyoyoni mwetu bado unaishi. Kwa vyovyote kifo hakitutenganishi na wapendwa wetu, tutaendelea kukukumbuka daima,"ameandika Zari kwenye akaunti yake ya Instagram.

Amesema, yeye na vijana wake watatu ambao ni George Semwanga, Dido Semwanga na  Pinto Semwanga, wataendelea kumkumbuka na anaamini Ivan Don anawaangalia na kufurahi huko alipo.

Ivan Don, alizaliwa Desemba 12, 1977 katika mji wa Kayunga, Uganda, amefariki Mei 25, 2017, katika hopitali ya Steve Biko Academic iliyopo Pretoria, Afrika Kusini nakuzikwa kwao Uganda.

Watoto ambao Zari alizaa na Ivan Don ni pamoja na George Semwanga, Dido Semwanga na Pinto Semwanga. Lakini baadaye Zari alizaa na msanii wa Bongo Fleva, Abdul Naseeb 'Diamond' ambao ni Latifah Dangote na Nillan 'Prince Nillan'.