Zari amkaushia Diamond Platnumz siku yake ya kuzaliwa

Muktasari:

Kwa hali hiyo bado hali inaonekana mambo si shwari hasa kutokana na siku kadhaa Zari kuweka posti za vijembe ambazo zinaonekana wazi zilikuwa zinaenda upande wa pili wa Diamond Platnumz.

Dar es Salaam. Hali inayoendelea kwa sasa mtandaoni bado ni utata hasa baada ya Zari mpaka sasa hajamtakia heri ya kuzaliwa Diamond Platnumz katika kurasa zake za mitandao ya kijamii kama alivyofanya Diamond kwake.
Kwa hali hiyo bado hali inaonekana mambo si shwari hasa kutokana na siku kadhaa Zari kuweka posti za vijembe ambazo zinaonekana wazi zilikuwa zinaenda upande wa pili wa Diamond Platnumz.
Lakini jambo jema ni kwa jinsi Wema Sepetu alivyoweza kumtakia heri Diamond katika kurasa yake ya Instagram na pia Mond naye kujibu katika komenti hali ambayo imezidi kuwafurahisha zaidi mashabiki wa pande hizo mbili ambao kwa miaka kadhaa walikuwa paka na panya.