Wema apata mzuka

Muktasari:

Katika kujijenga zaidi, wiki iliyopita Wema alijiunga na Chama cha Waigizaji wa Mkoa wa Kinondoni, ikiwa ni juhudi za kujitanua zaidi kisanaa.

NYOTA wa filamu za Bongo, Wema Sepetu, anaamini Tuzo ya Sinema Zetu aliyoshinda wiki chache zilizopita, imefungulia njia ya kupata tuzo nyingine nyingi kwa siku zijazo.

Katika kujijenga zaidi, wiki iliyopita Wema alijiunga na Chama cha Waigizaji wa Mkoa wa Kinondoni, ikiwa ni juhudi za kujitanua zaidi kisanaa.

“Nilikuwa nafanya filamu kama kitu tu cha ziada, ila sasa nimeamua kuifanya kuwa kazi rasmi. Tuzo imenitia mzuka na nimeamua kujiunga kwenye chama ili nifanye kazi,”alisema Wema ambaye ni Miss Tanzania wa mwaka 2006.

Katika hatua nyingine, Wema, alisema kwa sasa yupo katika mazungumzo na baadhi ya vituo vya televisheni kwa ajili ya kutengeneza tamthilia huku akijipanga pia kurekodi filamu mbili au tatu tu kwa mwaka kwani anaamini atakuwa na muda mdogo wa kupumzika.