We Dogo Janja shauri yako

Friday June 23 2017

 

RAPA Dogo Janja naye kalizua jamani. Wiki hii amekumbwa na madai ya kujihusisha kimapenzi na mrembo Munalove, jambo ambalo limezua hali ya sintofahamu kwa kuwa kiumri rapa huyo ni mdogo.

Madai hayo ndiyo habari ya mtandaoni huku mashabiki wa Dogo Janja wakisema kama ni kweli, basi Dogo Janja asipoangalia anaweza kupotea kimuziki kwa kujiingiza katika mapenzi mapema, tena kwa wanawake wanaomzidi umri.

Wengine wanasema eti si mara ya kwanza kwa Dogo Janja kujihusisha kimapenzi na wasanii waliomzidi umri. Hata hivyo, kuna wanaomtetea wakisema hajaanza mambo hayo, bali kupiga nao picha au kuwa karibu nao ndicho kinachomponza na watu wanamsingizia tu.

Mwanaspoti lilizungumza na Dogo Janja na yeye amekanusha kuwa na uhusiano huo akisema ni habari za mashabiki hizo.