Wasanii wazusha vurugu msiba wa Masogange

Muktasari:

  • Kutokana na vurugu za watu wanaotaka kupiga picha na wasanii, shughuli zilisimama kwa muda kwa lengo la kusubiri askari wa kuimalisha ulinzi.

Mbeya. Wasanii mbalimbali waliohudhulia tukio hilo walikuwa kivutio kwa watu waliofika msibani nyumbani kwa Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa kila mmoja kutaka kupiga picha jambo lililosababisha ratiba kuvurugika.

Kutokana na vurugu za watu wanaotaka kupiga picha na wasanii, shughuli zilisimama kwa muda kwa lengo la kusubiri askari wa kuimalisha ulinzi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika aliwasili msibani hapo akiwa ameambatana na askari na kurudisha hali ya utulivu na shughuli kuendelea.

Awali Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya, Akim Mwalupini alisema sababu ya vijana wa CCM kuubeba mwili wa marehemu Masogange kuwa baba mzazi wa marehemu mzee Gerald Waya ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Utengule Usongwe.

 Pia, alisema marehemu Masogange alikuwa kada wa CCM hizo ndio sababu za msingi ambazo ni lazima CCM wahusike kwenye msiba huo.