Wakali wa Bongo Fleva kuja kivingine

Muktasari:

“Watu wajipange na ujio wetu wa hatari na tutawaonesha kwa nini muda wote tulikuwa kimya sababu tumejipanga vyema,”

Msanii aliyetamba na singo ya ‘Atatamani’ Makamua amesema kuwa kundi la Wakali Kwanza bado lipo na wana mpango wa kuja kinamna ya kipekee ambayo itawashangaza watu wengi.
“Watu wajipange na ujio wetu wa hatari na tutawaonesha kwa nini muda wote tulikuwa kimya sababu tumejipanga vyema,”
“Muziki wa sasa inabidi kujipanga vyema sana ndio maana unaona tupo kimya sana sababu hatutaki kuja kuharibu, tunataka kuja kuleta kitu kizuri zaidi tofauti na mwanzo na tulete ladha nyingine pia,” aliongeza.
Pia, Makamua anasema amejipanga vizuri kwa upande wake kuja kinamna tofauti ukiachana na kundi lao huku akithibitisha kuwa anasubiri menejimenti yake itoe Baraka kwaajili ya kuachia kazi mbalimbali.