Usher Raymond katika kashfa mpya

Wednesday September 6 2017

 

By FRANK NGOBILE

Wakati kashfa yake ya kuwaambukiza magonjwa ya zinaa wanawake ikiwa bado haijapoa mwanamuziki Usher Raymond ameingia katika kashfa nyingine ya kucheza picha za ngono na mmoja wa wasaidizi.

Msichana Quantasia Sharpton katika mahojiano yake na mtandao wa YouTube vlogger Miss Jacob Kohinoor amesema ana ushahidi  wa video ya ngono waliyorekodi na Usher aliyekuwa anajua kuhusiana na hiyo.

Anaongeza kuwa wakili wake Lisa Bloom tayari ameshatembelea hoteli ya  Subpoena Hotel ambayo inasemekana shughuli nzima ilifanyika hapo na tayari wamepata baadhi ya video zikimuonesha Usher akiwa anaelekea kwenye chumba ambacho alikuepo Quantasia mwaka 2014.

Moja ya wafanyakazi wa zamani katika hoteli hiyo alikaliliwa akisema kuwa, alimuona Usher katika hoteli hiyo muda ya jioni na baadae alikuja mwanamke ambaye ndiye Quantasia kumchukua na kuelekea katika chumba ambacho alifikia awali Quantasia.

Madai hayo yamepingwa na Usher aliyesema wakati huo alikuwa bize na penzi la mpenzi wake kwa kipindi hicho ambae sasa ni mke wake na zaidi kuongeza kuwa Quantasia siyo aina ya wanawake anaoweza kutoka nao kimapenzi hata kidogo.