Ujumbe wa Kanye wamchanganya Kim

Muktasari:

  • Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika, “Wakati mwingine ni heri kuacha vitu vyote.”

UNAAMBIWA Rapa, Kanye West amerudi kwa kishindo kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kurusha vijembe.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika, “Wakati mwingine ni heri kuacha vitu vyote.”

Ujumbe huo ulimshtua Kim ambaye alishindwa kuvumilia na kujikuta akimjibu, “ Subiri, kila kitu?” Chrissy Teigan aliingilia kati na kumtania Kim, “ Nyumbani kwangu kuna nafasi unaweza ukaja na watoto,”

Kim akamjibu, “Asante kwa kujali rafiki yangu, labda amemaanisha kila kitu hata sisi familia yake.”