Tristan nusura anyimwe mtoto

Muktasari:

  • Chanzo cha habari kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Khloe amekuwa akifikiria kumpa mtoto wake jina la pili la baba yake kutokana na kashfa ya usaliti.

NYOTA wa mpira wa kikapu Marekani, Tristan Thompson chupuchupu anyimwe haki ya jina lake kutumika kwa mtoto wake aliyezaa na Khloe Kardashian.

Chanzo cha habari kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Khloe amekuwa akifikiria kumpa mtoto wake jina la pili la baba yake kutokana na kashfa ya usaliti.

Wiki iliyopita video iliyomuonyesha Tristan akiwa kimahaba na wanawake wawili. Video hiyo ilisambazwa ikiwa zimesalia saa chache kabla ya Khloe kujifungua mtoto wa kike aitwaye True.

Licha ya kuwa Khloe hakutaka kuonyesha hasira yake hadharani inadaiwa alipata wakati mgumu kuamua jina la pili la mtoto wake lisomeke Tristan au Kardashian.

Lakini baadaye aliamua cheti cha mtoto wake kiandikwe True Tristan. Wakati hayo yakiendelea familia ya Kardashian imemtaka ndugu yao kurudi Los Angeles. Familia hiyo imeshindwa kuficha hasira yake dhidi ya Tristan kwa kitendo cha kumsaliti ndugu yao tena akiwa mjamzito. Msimamo wa Khloe ataenda Los Angeles baada ya Tristan kumaliza mechi zake.