Dogo Janja afunguka mapenzi yake kwa Vanessa

Tuesday October 10 2017

 

By FRANK NGOBILE

MKALI wa Bongo Fleva Dogo Janja amefunguka wazi juu ya mapenzi yake kwa Vanessa Mdee hasa kwa jinsi ambavyo anavaa na kusema anatamani kuona hata kina dada wengine wakipiga mizigo kama Vanessa.
Dogo Janja ambaye amekuwa akihusishwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Uwoya madai ambayo ameyakana na kudai yeye ana mwanamke wake ambaye hayupo kabisa kwenye sanaa na kuongeza kuwa, Vee humkosha zaidi.
“Kiukweli huwa nazimia sana swagga za Vee Money, anajua kupendeza na kuna wakati huwa natamani mastaa wa kike wote wavae na kutupia pamba kama yeye,” alisema Dogo Janja.