Mashabiki wamkomalia Stereo kufyatua remix

Tuesday October 10 2017

 

By FRANK NGOBILE

MKALI ambaye anatamba na Mpe Habari ambayo alifanya na mkali mwingine kutoka Wasafi Rich Mavoko, Stereo amesema kuwa ujio wa remix mpya ambayo amewaongeza wakali Jay Mo, Khaligraph Jones, Stamina na Billnas hakutaka kuja kwa remix hiyo.
“Sikutaka kuja kwa remix mimi nilitaka nije na wimbo mwingine kabisa lakini watu wakahitaji na mtu kama Khaligraph Jones ndio mtu wa kwanza kuniambia anatamani itokee remix,”
“Na pia nilipomuambia juu ya ujio wa remix alikuwa mtu wa kwanza kabisa kunitumia mashairi yake mpaka nikashangaa lakini kiukweli mimi sikuwa na mpango huo bali baadhi ya watu,” aliongeza zaidi.
Pia stereo aliongeza kuwa watu waendelee kusubiri mambo mengi mazuri kutoka kwake japo amebanwa na kazi ambayo amesema inamuwia muda mgumu kuweka kufanya yote kwa pamoja.