Siamini kama kuna mtu anapenda ubaya

Tuesday November 28 2017

 

MLIMBWENDE wa filamu za Bongo, Wema Sepetu maarufu kama Madame amewataka wasanii wenzake na Watanzania kwa ujumla kuacha kuombeana mabaya kwani hakuna anayepanda kutana na vikwazo katika maisha yake.

“Mtu amepatwa na matatizo anatakiwa apate faraja lakini si kuonyesha hisia za hasira au kufurahia. Hakuna ambaye anaweza kujua kuwa ni siku gani anaweza akawa sehemu ambayo hakupanga,” alisema Wema.

Anaamini kuwa hata yule anayekuonyesha kuwa ni rafiki ipo siku atakukana na kuwa adui wako, huku pia wengine wakijificha na kufurahia matatizo yako nyuma ya pazia.