Shilole apigwa na mumewe

Tuesday March 13 2018

 

By Rhobi Chacha

MSANII wa Bongo Fleva Shilole, hivi majuzi amedaiwa kupigwa na mumewe, Uchebe baada ya kutuhumiwa kumdhalilisha katika pati moja walioalikwa maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.

Ipo hivi: Shilole na Uchebe walialikwa kwenye pati hiyo ambayo ilishuhudiwa Shilole akicheza muziki huku akionyesha baadhi ya maungo yake. Ndipo Uchebe akamwambia ajistiri, lakini Shilole hakutaka kusikia na kumpa mumewe maneno ya kashfa kwa kumwambia asiongee kitu kwani yeye ndiye amemuoa.

Baada ya hapo, Uchebe aliondoka na kumsubiri nyumbani na aliporejea alimpiga baada ya kuona pia kwenye akaunti ya mtu mwingine Shilole akicheza baada ya yeye kuondoka. Baada ya kipigo hicho Shilole aliondoka na kwenda kulala Gesti.

Alipoulizwa kuhusu sakata hilo, Shilole alikiri kupigwa ila chanzo sio cha kucheza muziki bali, ni mumewe Uchebe kumhisi anatoka kimapenzi na Mtangazaji Sudy Brouwn.