Wazaramo waliamsha dude Zanzibar

Sunday February 11 2018

 

By Rhobi Chacha

Zanzibar. Kikundi cha ngoma  za asili ya Kizaramo kutoka Tanzania, Segere Original wameweza kuamsha furaha kwa mashabiki zao kwa kutoa burudani ya muziki wa asili unaofanywa na kikundi hicho katika Tamasha la Sauti za busara 2018

Kikundi hicho ambacho kilianzishwa zaidi ya miaka kumi iliyopita,kimesema hakuna vikundi viwili vya Segere kama baadhi ya watu wanavyodhani, ila kuna Segere na Young Star ya Siza Mogela ndio wanadhani ni Segere nyingine.


Aidha walifafanua zaidi kwa kusema, neno Segere  limetokana na wimbo waliowahi kuuimba hapo nyuma hivyo wakaona bora walitumie  liwe jina la kundi.

Wakati huo huo kundi hilo limeweza kumtambulisha kijana wao mdogo anayefanya muziki wa Singeli aitwaye Elisha Dafa maarufu kama Dogo Elisha.