Saida Karoli aonyesha umahiri wake Sauti za Busara

Sunday February 11 2018

 

By Rhobi Chacha

Zanzibar. Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amedhilirisha uwezo wake wa kulitawala jukwaa kwa kuimba na kucheza katika tamasha la muziki la Sauti za Busara kwa mwaka 2018.
Saida ambaye amekuwa kivutia usiku wa jana ameweza kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuimba vibao vyake matata kama vile;- ‘Malia Salome,’ Orugambo’   Mapenzi Kizunguzungu’ na nyinginezo
Msanii huyo alikuwa miongoni mwa wasanii waliotambulishwa na waandaji wa shindano hilo kutumbuiza tamasha la msimu huu.