Roma, Darasa kukinukisha Sikukuu ya Eid

Muktasari:

Burudani hiyo itaanza asubuhi saa nne kwa watoto, huku wakicheza michezo ya kuogelea, baiskeli na bembea wakisindikizwa na burudani kutoka kwa Wakali Dancer.

Dar es Salaam. Wasanii wa kizazi kipya Roma Mkatoliki, Darasa, Mr Blue, Stamina, Snura Majanga na Zanzibar Stars kutoa burudani ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Rangi Tatu katika Sikukuu ya Eid Mosi.

Burudani hiyo itaanza asubuhi saa nne kwa watoto, huku wakicheza michezo ya kuogelea, baiskeli na bembea wakisindikizwa na burudani kutoka kwa Wakali Dancer.

Baada ya hapo kuanzia saa mbili usiku mpaka asubuhi kutakuwa na burudani ya wakubwa.