Ray ataka mambo hadharani

Muktasari:

  • Ray amesema wasanii wajifunze kusema ukweli, pindi wanapokuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwani hata wao wasanii ni binadamu pia haina haja ya kujificha kuwaogopa watu.

MWIGIZAJI wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ amewashauri waigizaji wenzake na kuwaomba pindi wanapokuwa katika uhusiano wa kimapenzi, basi wawe wawazi na kuacha uongo.

Ray amesema wasanii wajifunze kusema ukweli, pindi wanapokuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwani hata wao wasanii ni binadamu pia haina haja ya kujificha kuwaogopa watu.

“Kusema uongo ni dhambi, na mficha maradhi kifo humuumbua,kwani hakuna uongo unaoweza kudumu milele, “ alisema Ray.

Ray kwa sasa ana mtoto mmoja wa kiume, aliyezaa na mwigizaji wa filamu, Chuchu Hans.