Rado aushtukia mchezo mapema tu

Tuesday October 10 2017

 

MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu nchini, Simon Mwapagata ‘Rado’ anaamini Bongo Movie haijashuka, ila kulikuwa na mapungufu yaliyoporomosha soko lakini sasa watu wamejirekebisha.

Rado alisema wajanja wameshtuka na kurejea kutengeneza kazi zenye ubora na zinazoendana na uhalisia, ili kuwapa mashabiki wao kitu wanachokitaka. Anasisitiza na yeye ni mmoja wao.

“Wapenzi wa filamu wanataka vitu tofauti, sio kuangalia kazi zile zile. Ukiangalia hata kazi yangu mpya utagundua, nina nia ya dhati kuiamsha Bongo Movie,” alisema Rado.

Msanii huyo aliyeizindua filamu yake hiyo katika ukumbi wa Mlimani City na kuwa gumzo, anasema alifanya hivyo ikiwa ni moja ya njia ya kukuza sokao la filamu na kuwashauri watayarishaji wengine kupanua masoko ili wafike mbali.