Rachel amkana TID

Muktasari:

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Same Boy’ alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na wala hajawahi kubeba ujauzito wa TID.

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Bongo, Rachel amesema hajawahi kutoka kimapenzi na TID kama inavyokuwa ikiripotiwa awali.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Same Boy’ alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na wala hajawahi kubeba ujauzito wa TID.

“Niseme tu TID siyo bwana yangu, siyo mtu wangu, TID hawezi kuwa mtu wangu, TID mkubwa ujue, ana type zake, mimi nina type zangu za wanaume ambao natakiwa ni date nao, TID siyo type ya wanaume ambao naweza ku-date nao, kirafiki kuongea sawa.”

“Naomba nieleweke, sijawahi kutoka kimapenzi na TID, sijawahi kubeba mimba ya TID hata mara moja,” amesisitiza Rachel