Nimesema sitaki, sitaki mkome!

Saturday July 1 2017

 

SOSHIOLAITI maarufu nchini Huddah Monroe kafunguka ya moyoni kwa kudai kuwa  amechoshwa na usumbufu wa ma-ex wake wanaoshinda kumtafuta kila wakati kwa kuwa hawataki kukubalia kuwa waliachana.

Akifungua roho,  mrembo huyo ambaye hivi majuzi alikuwa nchini Equatorial Guinnea kwa mwaliko wa kuhudhuria sherehe ya bethidei ya naibu Rais wa taifa hilo, Teodoro Nguema Obiang, kasema anajutia sana kuwahi kutoka na baadhi ya ma-ex wake hao waliogeuka kuwa kero kubwa katika maisha yake na simu zao za ‘kipuzi’.“

Kama kipo kitu kimoja ninachojutia sana maishani mwangu, ni baadhi ya watu ambao kama ningelijua singedhubutu kutoka nao kimapenzi.

Sijui kama ningelipata ujauzito wao ingelikuweje, ningeishi kujilaani. Wamegeuka kuwa kero kwangu sasa, unakuta kipindi najitahidi kuwasahau, ndipo nao wapo bize kunipigia simu kila wakati eti wakidai wananijulia hali wakati wakijua ninavyochukia nafsi zao” Huddah katiririka.

Tofauti na zamani, siku hizi maisha ya Huddah hayaeleweki hasa ya kimapenzi baada yake kubadilika na kuamua kuyafanya kuwa siri tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma kidogo.