Nicki Minaj: Usiweke Mchezo na Albamu Yangu Mpya

Tuesday September 12 2017

 

By FRANK NGOBILE

Mwanadada kutoka Young Money, Nicki Minaj kathibitisha juu ya ujio wa albamu yake ya nne huku akiimwagia sifa kede kede kuwa itakua si ya mchezo.
Aliongea hayo usiku akiwa anatoka katika tamasha la fasheni katika jiji la New York mbele ya mashabiki zake kadhaa ambapo kwa sauti aliwaambia kua Albamu inayokuja ni balaa sana.
Mwezi juni mwaka huu aliongea juu ya ujio wa albamu yake ya nne, ambapo alisema kua anampango wa kufanya kazi ambayo itakua ya kihistoria katika ulimwengu wa wapenzi wa Hip Hop na watu hawatasahau.
"Kinachofuata sasa ni kuachia albamu yangu ya nne na nitahakikisha inakua albamu bora na watu hawatasahau kamwe"
"Najua itakua moja ya kazi zangu bora na siku zote napenda kufanya kazi katika wakati sahihi, napenda mashabiki zangu wakifurahia kitu fulani kutoka kwangu" aliongeza.
"Na kwa sasa ndicho ninachokiangalia, kufanya kazi nzuri ambayo itakua ni shukrani kwa watu wote waliokua nami kwa miaka yangu yote" alimaliza
Tangu mwaka 2016 akiwa kwenye mahusiano na rapa Meek Mill, ujio wa albamu yake ulikua ukiongelewa sana na mara kadhaa alikaliliwa akithibitisha juu ya maandalizi ya albamu yake.
Baada ya kuachana na Rapa huyo Nicki ameonekana akiwa na baadhi ya wasanii kadhaa kama Quavo ambapo wameonekana  wakiandaa kazi kadhaa na tayari inathibitika kua wamekwisha shuti video ambayo inatazamiwa kuachiwa muda wowote kuanzia sasa.
Yote na yote, bado watu wanasubiri kwa hamu juu ya ujio wa albamu hiyo ambayo bado haijafahamika lini inaachiwa.