Ndoa ya Prince Harry yaiva

Muktasari:

  • Jarida la Us weekly limeandika kuwa tayari wageni wote waalikwa wameshafikishiwa mialiko yao tayari kwa ajili ya kuhudhuria harusi hiyo.

ZIKIWA zimesalia siku kadhaa kabla ya kufungwa kwa ndoa ya kifalme kati ya Prince Harry na Meghan Markle, maandalizi ya harusi hiyo yamekamilika.

Jarida la Us weekly limeandika kuwa tayari wageni wote waalikwa wameshafikishiwa mialiko yao tayari kwa ajili ya kuhudhuria harusi hiyo.

Meghan naye anaendelea na taratibu za kuhamishia makazi yake nchini Uingereza katika jumba la kifalme.

Harusi hiyo itakayofanyika mwezi ujao na itahudhuriwa na watu maarufu duniani.